×

Mali aliyo leta Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake kutoka kwa watu wa 59:7 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-hashr ⮕ (59:7) ayat 7 in Swahili

59:7 Surah Al-hashr ayat 7 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-hashr ayat 7 - الحَشر - Page - Juz 28

﴿مَّآ أَفَآءَ ٱللَّهُ عَلَىٰ رَسُولِهِۦ مِنۡ أَهۡلِ ٱلۡقُرَىٰ فَلِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ وَلِذِي ٱلۡقُرۡبَىٰ وَٱلۡيَتَٰمَىٰ وَٱلۡمَسَٰكِينِ وَٱبۡنِ ٱلسَّبِيلِ كَيۡ لَا يَكُونَ دُولَةَۢ بَيۡنَ ٱلۡأَغۡنِيَآءِ مِنكُمۡۚ وَمَآ ءَاتَىٰكُمُ ٱلرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَىٰكُمۡ عَنۡهُ فَٱنتَهُواْۚ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَۖ إِنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلۡعِقَابِ ﴾
[الحَشر: 7]

Mali aliyo leta Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake kutoka kwa watu wa hivi vijiji ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na kwa ajili ya Mtume, na jamaa, na mayatima, na masikini, na msafiri, ili yasiwe yakizunguka baina ya matajiri tu miongoni mwenu. Na anacho kupeni Mtume chukueni, na anacho kukatazeni jiepusheni nacho. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ما أفاء الله على رسوله من أهل القرى فلله وللرسول ولذي القربى, باللغة السواحيلية

﴿ما أفاء الله على رسوله من أهل القرى فلله وللرسول ولذي القربى﴾ [الحَشر: 7]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Hayo mali ya washirikina wa watu wa miji ambayo Mwenyezi Mungu Amewaletea bila kupanda farasi wala ngamia, basi hayo ni ya Mwenyezi Mungu na ya Mtume Wake, yatatumiwa kwa maslahi ya Waislamu kwa jumla, jamaa wa karibu wa Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na mayatima: nao ni watoto maskini waliofiliwa na baba zao, maskini: nao ni wenye uhitaji na ufukara, na ibn al-sabīl: naye ni mgeni msafiri ambaye matumizi yake yameisha na mali yake yamemalizika. Hiyo ni kwa sababu mali yasiwe ni milki inayozunguka kwa matajiri peke yao, na mafukara na maskini wakanyimwa nayo. Na mali yoyote ambayo Mtume Amewapatia au sheria yoyote aliyowawekea, basi chukueni, na chochote kile alichowakataza basi komekeni nacho. Na muogopeni Mwenyezi Mungu kwa kufuata amri Zake na kuepuka makatazo Yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye mateso makali kwa anayemuasi na kuenda kinyume na amri Yake na makatazo Yake. Na aya hii ni msingi wa ulazima wa kufuata Sunnah iwe ni ya maneno, ya vitendo au ya kukubali jambo lifanyike kwa kutolikataza
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek