Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 110 - الأنعَام - Page - Juz 7
﴿وَنُقَلِّبُ أَفۡـِٔدَتَهُمۡ وَأَبۡصَٰرَهُمۡ كَمَا لَمۡ يُؤۡمِنُواْ بِهِۦٓ أَوَّلَ مَرَّةٖ وَنَذَرُهُمۡ فِي طُغۡيَٰنِهِمۡ يَعۡمَهُونَ ﴾
[الأنعَام: 110]
﴿ونقلب أفئدتهم وأبصارهم كما لم يؤمنوا به أول مرة ونذرهم في طغيانهم﴾ [الأنعَام: 110]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na tutazigeuza nyoyo zao na macho yao, tuweke kizuizi baina yake na kunufaika na alama za Mwenyezi mungu, wasiziamini kama walivyokuwa hawakuziamini aya za Qur’ani zilipoteremka kwa mara ya kwanza, na tutawaacha wao wameduwaa katika kumuasi kwao Mwenyezi Mungu, hawaongoki kwenye haki na usawa |