Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 111 - الأنعَام - Page - Juz 8
﴿۞ وَلَوۡ أَنَّنَا نَزَّلۡنَآ إِلَيۡهِمُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةَ وَكَلَّمَهُمُ ٱلۡمَوۡتَىٰ وَحَشَرۡنَا عَلَيۡهِمۡ كُلَّ شَيۡءٖ قُبُلٗا مَّا كَانُواْ لِيُؤۡمِنُوٓاْ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَهُمۡ يَجۡهَلُونَ ﴾
[الأنعَام: 111]
﴿ولو أننا نـزلنا إليهم الملائكة وكلمهم الموتى وحشرنا عليهم كل شيء قبلا﴾ [الأنعَام: 111]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na lau kama sisi tungaliyaitikia maombi ya washirikina hawa na kuwateremshia Malaika kutoka mbinguni na tukawafufulia wafu wakazungumza nao na tukawakusanyia kila kitu walichokitaka wakakiona ana kwa ana, hawangaliyakubali yale uliyowaitia, ewe Mtume, na hawangaliyatumia, isipokuwa yule ambaye Mwenyezi Mungu Alimtakia uongofu. Lakini wengi wa hawa makafiri hawaijui haki ambayo umekuja nayo kutoka kwa Mwenyezi Mungu |