×

Wala msile katika wale wasio somewa jina la Mwenyezi Mungu. Kwani huo 6:121 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-An‘am ⮕ (6:121) ayat 121 in Swahili

6:121 Surah Al-An‘am ayat 121 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 121 - الأنعَام - Page - Juz 8

﴿وَلَا تَأۡكُلُواْ مِمَّا لَمۡ يُذۡكَرِ ٱسۡمُ ٱللَّهِ عَلَيۡهِ وَإِنَّهُۥ لَفِسۡقٞۗ وَإِنَّ ٱلشَّيَٰطِينَ لَيُوحُونَ إِلَىٰٓ أَوۡلِيَآئِهِمۡ لِيُجَٰدِلُوكُمۡۖ وَإِنۡ أَطَعۡتُمُوهُمۡ إِنَّكُمۡ لَمُشۡرِكُونَ ﴾
[الأنعَام: 121]

Wala msile katika wale wasio somewa jina la Mwenyezi Mungu. Kwani huo ni upotofu. Na kwa yakini mashet'ani wanawafunza marafiki zao kubishana nanyi. Na mkiwafuata basi hapana shaka nyinyi mtakuwa washirikina

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ولا تأكلوا مما لم يذكر اسم الله عليه وإنه لفسق وإن الشياطين, باللغة السواحيلية

﴿ولا تأكلوا مما لم يذكر اسم الله عليه وإنه لفسق وإن الشياطين﴾ [الأنعَام: 121]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na wala msile, enyi Waislamu, katika vichinjwa, yule ambaye halikutajwa jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kuchinjwa, kama mfu na aliochinjiwa masanamu na majini na wasiokuwa hao. Na kwa hakika kuwala wanyama hao ni kutoka kwenye twaa ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka. Na majini waasi wanawatia marafiki zao, miongoni mwa mashetani wa kibinadamu, ushawiwishi wa kuwatatiza kuhusu uharamu wa kula mfu; wanawaamrisha wawaambie Waislamu wanapobishana nao, «Hakika nyinyi, kwa kutokula kwenu mfu, huwa hamli anachokiua Mwenyezi Mungu, ambapo mnakula mnachokichinja.» Na iwapo mtawasikiliza, enyi Waislamu, katika kuhalalisha mfu, basi nyinyi mtakuwa sawa na wao katika ushirikina
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek