Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 14 - الأنعَام - Page - Juz 7
﴿قُلۡ أَغَيۡرَ ٱللَّهِ أَتَّخِذُ وَلِيّٗا فَاطِرِ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ وَهُوَ يُطۡعِمُ وَلَا يُطۡعَمُۗ قُلۡ إِنِّيٓ أُمِرۡتُ أَنۡ أَكُونَ أَوَّلَ مَنۡ أَسۡلَمَۖ وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ ﴾
[الأنعَام: 14]
﴿قل أغير الله أتخذ وليا فاطر السموات والأرض وهو يطعم ولا يطعم﴾ [الأنعَام: 14]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na asiyekuwa Yeye, «Je, nimchukue asiyekuwa Mwenyezi Mungu kuwa ni msaidizi na ni mwokozi, na hali Yeye ni Muumba mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake, na Yeye Ndiye Mwenye kuwaruzuku viumbe Wake na hakuna mwenye kumruzuku Yeye?» Sema,ewe Mtume, «Mimi nimeamrishwa niwe ni wa mwanzo aliyemnyenyekea Yeye na kumwandama katiika umma huu. Na nimekatazwa kuwa ni miongoni mwa wanaomshirikisha Yeye na asiyekuwa Yeye |