Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 13 - الأنعَام - Page - Juz 7
﴿۞ وَلَهُۥ مَا سَكَنَ فِي ٱلَّيۡلِ وَٱلنَّهَارِۚ وَهُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ ﴾
[الأنعَام: 13]
﴿وله ما سكن في الليل والنهار وهو السميع العليم﴾ [الأنعَام: 13]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Ni wa Mwenyezi Mungu umiliki wa kila kitu, kilicho mbinguni na ardhini, kilichotulia na kinachotembea, kilichofichika na kilicho wazi. Vyote ni watumwa Wake na viumbe Vyake na viko chini ya utendeshaji nguvu Wake, uendeshaji Wake na upangaji Wake. Yeye Ndiye Msikizi wa maneno ya waja Wake, Ndiye Mjuzi wa siri zao na matendo yao |