×

Na Yeye ndiye aliye ziumba bustani zenye kutambaa juu ya chanja, na 6:141 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-An‘am ⮕ (6:141) ayat 141 in Swahili

6:141 Surah Al-An‘am ayat 141 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 141 - الأنعَام - Page - Juz 8

﴿۞ وَهُوَ ٱلَّذِيٓ أَنشَأَ جَنَّٰتٖ مَّعۡرُوشَٰتٖ وَغَيۡرَ مَعۡرُوشَٰتٖ وَٱلنَّخۡلَ وَٱلزَّرۡعَ مُخۡتَلِفًا أُكُلُهُۥ وَٱلزَّيۡتُونَ وَٱلرُّمَّانَ مُتَشَٰبِهٗا وَغَيۡرَ مُتَشَٰبِهٖۚ كُلُواْ مِن ثَمَرِهِۦٓ إِذَآ أَثۡمَرَ وَءَاتُواْ حَقَّهُۥ يَوۡمَ حَصَادِهِۦۖ وَلَا تُسۡرِفُوٓاْۚ إِنَّهُۥ لَا يُحِبُّ ٱلۡمُسۡرِفِينَ ﴾
[الأنعَام: 141]

Na Yeye ndiye aliye ziumba bustani zenye kutambaa juu ya chanja, na zisio tambaa, na mitende, na mimea yenye matunda mbali mbali, na mizaituni na mikomamanga inayo fanana na isiyo fanana. Kuleni matunda yake inapo zaa, na toeni haki yake siku ya kuvunwa kwake. Wala msitumie kwa fujo. Hakika Yeye hawapendi watumiayo kwa fujo

❮ Previous Next ❯

ترجمة: وهو الذي أنشأ جنات معروشات وغير معروشات والنخل والزرع مختلفا أكله والزيتون, باللغة السواحيلية

﴿وهو الذي أنشأ جنات معروشات وغير معروشات والنخل والزرع مختلفا أكله والزيتون﴾ [الأنعَام: 141]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na Mwenyezi Mungu, kutkata na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, Ndiye Aliyewaanzishia mashamba: miongoni mwa mimea yake kuna ile iliyoinuliwa juu ya ardhi na kuegemezewa vitu vyingine, kama mizabibu, na miongoni mwayo kuna isiyoinuliwa, bali inasimama yenyewe kwenye vigogo vyake, kama mitende na miti mingine ya mazao. Mimea yote hiyo ikiwa ina tamu tafauti. Mizabibu na mikomamanga, maumbile yake yanafanana na matunda yake yanatafautiana tamu yake. Kuleni, enyi watu, matunda yake na mtoe Zaka zake zilizolazimishwa kwenu siku mnapoyavuna na kuyatungua, na msiikiuke mipaka ya usawa katika kutoa mali na kula chakula na mengineyo. Hakika Yeye, Mwenyezi Mungu, Hawapendi wenye kukiuka mipaka Yake kwa kutumia mali katika njia zisokuwa zake
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek