×

Sema: Njooni nikusomeeni aliyo kuharimishieni Mola wenu Mlezi. Nayo ni kuwa, msimshirikishe 6:151 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-An‘am ⮕ (6:151) ayat 151 in Swahili

6:151 Surah Al-An‘am ayat 151 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 151 - الأنعَام - Page - Juz 8

﴿۞ قُلۡ تَعَالَوۡاْ أَتۡلُ مَا حَرَّمَ رَبُّكُمۡ عَلَيۡكُمۡۖ أَلَّا تُشۡرِكُواْ بِهِۦ شَيۡـٔٗاۖ وَبِٱلۡوَٰلِدَيۡنِ إِحۡسَٰنٗاۖ وَلَا تَقۡتُلُوٓاْ أَوۡلَٰدَكُم مِّنۡ إِمۡلَٰقٖ نَّحۡنُ نَرۡزُقُكُمۡ وَإِيَّاهُمۡۖ وَلَا تَقۡرَبُواْ ٱلۡفَوَٰحِشَ مَا ظَهَرَ مِنۡهَا وَمَا بَطَنَۖ وَلَا تَقۡتُلُواْ ٱلنَّفۡسَ ٱلَّتِي حَرَّمَ ٱللَّهُ إِلَّا بِٱلۡحَقِّۚ ذَٰلِكُمۡ وَصَّىٰكُم بِهِۦ لَعَلَّكُمۡ تَعۡقِلُونَ ﴾
[الأنعَام: 151]

Sema: Njooni nikusomeeni aliyo kuharimishieni Mola wenu Mlezi. Nayo ni kuwa, msimshirikishe Yeye na chochote. Na wazazi wenu wafanyieni wema. Wala msiwauwe watoto wenu kwa sababu ya umasikini. Sisi tunakuruzukuni nyinyi na wao. Wala msikaribie mambo machafu, yanayo onekana, na yanayo fichikana. Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameharimisha kuiuwa, ila ikiwa kwa haki. Hayo amekuusieni ili myatie akilini

❮ Previous Next ❯

ترجمة: قل تعالوا أتل ما حرم ربكم عليكم ألا تشركوا به شيئا وبالوالدين, باللغة السواحيلية

﴿قل تعالوا أتل ما حرم ربكم عليكم ألا تشركوا به شيئا وبالوالدين﴾ [الأنعَام: 151]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Waambie, ewe Mtume, «Njooni niwasomee Yale Aliyoyaharamishia Mwenyezi Mungu: Msishirikishe pamoja na Mwenyezi Mungu kitu chochote, miongoni mwa viumbe Vyake katika kumuabudu Yeye; bali zielekezeni aina zote za ibada Kwake Yeye Peke Yake, kama kucha, kutaraji, kuomba na megineyo. Muwafanyie wema wazazi wawili kwa kuwasaidia, kuwaombea Mungu na mengineyo ya wema kama hayo Msiwaue watoto wenu kwa sababu ya ufukara uliowshukia, kwani Mwenyezi Mungu Anawaruzuku nyinyi na wao. Wala msiyasongelee madhambi makubwa yaliyo wazi na yaliyofichika. Na msiiue nafsi ambayo Mwenyezi Mungu Ameharamisha kuuawa, isipokuwa kwa njia ya haki, nayo ni kuchukuliwa kisasi kwa aliyeua, au kwa uzinifu baada ya kuoa au kuolewa, au kuacha Uislamu. Hayo yaliyotajwa ni miongoni mwa yale ambayo Mwenyezi Mungu Amewkataza nayo na Akawapa maagizo muyaepuke na ni miongoni mwa yale Aliyowaamrisha nyinyi kwayo. Amweausia nayo Mola wenu ili mupate kuyaitia akilini maamrisho Yake na Makatazo Yake
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek