Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 20 - الأنعَام - Page - Juz 7
﴿ٱلَّذِينَ ءَاتَيۡنَٰهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ يَعۡرِفُونَهُۥ كَمَا يَعۡرِفُونَ أَبۡنَآءَهُمُۘ ٱلَّذِينَ خَسِرُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ فَهُمۡ لَا يُؤۡمِنُونَ ﴾
[الأنعَام: 20]
﴿الذين آتيناهم الكتاب يعرفونه كما يعرفون أبناءهم الذين خسروا أنفسهم فهم لا﴾ [الأنعَام: 20]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Wale tuliowapa Taurati na Injili wanamjua Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, kwa sifa Zake zilizoandikwa kwao kama wanavyowajua watoto wao. Na kama ilivyo wao hawachanganyikiwi kuwajua watoto wao walio mbele yao kuwapambanua na wengine, vilevile Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, hachanganyiki na mwingine, kwa sababu ya uwazi wa sifa zake zilizo ndani ya vitabu vyao. Lakini wao walifuata matamanio yao, walipomkanusha Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na yale aliyokuja nayo, ndipo wakapata hasara nafsi zao |