Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 21 - الأنعَام - Page - Juz 7
﴿وَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّنِ ٱفۡتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا أَوۡ كَذَّبَ بِـَٔايَٰتِهِۦٓۚ إِنَّهُۥ لَا يُفۡلِحُ ٱلظَّٰلِمُونَ ﴾
[الأنعَام: 21]
﴿ومن أظلم ممن افترى على الله كذبا أو كذب بآياته إنه لا﴾ [الأنعَام: 21]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakuna yoyote mwenye udhalimu mbaya zaidi kuliko yule aliyemzulia Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, urongo na akadai kwamba Yeye Ana washirika katika ibada, au akadai kwamba Yeye Ana mtoto au mke, au akazikanusha hoja Zake na dalili ambazo kwazo Aliwapa nguvu Mitume Wake, amani iwashukie. Hakika ya mambo ni kwamba madhalimu waliomzulia Mwenyezi Mungu urongo hawafaulu na hawapati matakwa yao ulimwenguni wala Akhera |