Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 61 - الأنعَام - Page - Juz 7
﴿وَهُوَ ٱلۡقَاهِرُ فَوۡقَ عِبَادِهِۦۖ وَيُرۡسِلُ عَلَيۡكُمۡ حَفَظَةً حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءَ أَحَدَكُمُ ٱلۡمَوۡتُ تَوَفَّتۡهُ رُسُلُنَا وَهُمۡ لَا يُفَرِّطُونَ ﴾
[الأنعَام: 61]
﴿وهو القاهر فوق عباده ويرسل عليكم حفظة حتى إذا جاء أحدكم الموت﴾ [الأنعَام: 61]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Ndiye Al-Qāhir (Mtendesha nguvu), Aliye juu ya waja Wake, ujuu wa kila namana usio na mipaka unaonasibiana na utkufu Wake, kutakata na kila sifa mbaya ni Kwake na kutukuka ni Kwake. Kila kitu kinaunyenyekea utukufu Wake na ukubwa Wake. Yeye Anawatuma kwa waja Wake Malaika kuyadhibiti matendo yao na kuyahesabu. Mpaka kifo kinapomshukia mmoja wao, Malaika wa mauti na wasaidizi wake wanaichukua roho yake, na wao hawaachi kutekeleza walichoamrishwa kukifanya |