Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 89 - الأنعَام - Page - Juz 7
﴿أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ ءَاتَيۡنَٰهُمُ ٱلۡكِتَٰبَ وَٱلۡحُكۡمَ وَٱلنُّبُوَّةَۚ فَإِن يَكۡفُرۡ بِهَا هَٰٓؤُلَآءِ فَقَدۡ وَكَّلۡنَا بِهَا قَوۡمٗا لَّيۡسُواْ بِهَا بِكَٰفِرِينَ ﴾
[الأنعَام: 89]
﴿أولئك الذين آتيناهم الكتاب والحكم والنبوة فإن يكفر بها هؤلاء فقد وكلنا﴾ [الأنعَام: 89]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Manabii hao tuliowaneemesha kwa uongofu na unabii, ndio wale tuliowapa Kitabu, kama vile kurasa za Ibrāhīm, Taurati ya Muūsā, Zaburi ya Dāwūd na Injili ya Īsā. Na tuliwapa ufahamu wa Vitabu hivi na tukawateua kufikisha wahyi wetu. Na iwapo makafiri wa watu wako, ewe Mtume, watazikanusha aya za hii Qur’ani, basi tumewategemezea watu wengine jambo hilo, - yaani: Muhājirūn (masahaba waliohamia Madina pamoja na Mtume) na Ans,ār (masahaba wenyeji wa Madina) na wafuasi wao mpaka Siku ya Kiyama- ambao hawatakuwa ni wenye kuzikanusha. Bali watakuwa ni wenye kuziamini, ni wenye kuzitumia |