Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 95 - الأنعَام - Page - Juz 7
﴿۞ إِنَّ ٱللَّهَ فَالِقُ ٱلۡحَبِّ وَٱلنَّوَىٰۖ يُخۡرِجُ ٱلۡحَيَّ مِنَ ٱلۡمَيِّتِ وَمُخۡرِجُ ٱلۡمَيِّتِ مِنَ ٱلۡحَيِّۚ ذَٰلِكُمُ ٱللَّهُۖ فَأَنَّىٰ تُؤۡفَكُونَ ﴾
[الأنعَام: 95]
﴿إن الله فالق الحب والنوى يخرج الحي من الميت ومخرج الميت من﴾ [الأنعَام: 95]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakika Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Anapasua mbegu ukatoka mmea, na Anapasua koko ukatoka mti. Anatoa chenye uhai kutokana na kilichokufa, kama vile binadamu na mnyama kutokana na tone la manii ya binadamu na mnyama. Na Anatoa kilichokufa kutokana na chenye uhai, kama tone la manii linalotokana na binadamu na mnyama. Huyo Ndiye Mwenyezi Mungu. Yaani Mwenye kufanya hili ni Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Asiye na mshirika, Anayestahiki kuabudiwa. Basi vipi nyinyi mtaepushwa na haki mpelekwe kwenye batili mkamuabudu pamoja na Yeye mwingine asiyekuwa Yeye |