×

Ndiye anaye pambazua mwangaza wa asubuhi; na ameufanya usiku kwa mapumziko na 6:96 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-An‘am ⮕ (6:96) ayat 96 in Swahili

6:96 Surah Al-An‘am ayat 96 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-An‘am ayat 96 - الأنعَام - Page - Juz 7

﴿فَالِقُ ٱلۡإِصۡبَاحِ وَجَعَلَ ٱلَّيۡلَ سَكَنٗا وَٱلشَّمۡسَ وَٱلۡقَمَرَ حُسۡبَانٗاۚ ذَٰلِكَ تَقۡدِيرُ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡعَلِيمِ ﴾
[الأنعَام: 96]

Ndiye anaye pambazua mwangaza wa asubuhi; na ameufanya usiku kwa mapumziko na utulivu, na jua na mwezi kwenda kwa hisabu. Hayo ndiyo makadirio ya Aliye tukuka Mwenye nguvu, Mwenye ujuzi

❮ Previous Next ❯

ترجمة: فالق الإصباح وجعل الليل سكنا والشمس والقمر حسبانا ذلك تقدير العزيز العليم, باللغة السواحيلية

﴿فالق الإصباح وجعل الليل سكنا والشمس والقمر حسبانا ذلك تقدير العزيز العليم﴾ [الأنعَام: 96]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na Mwenyezi Mungu, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, Ndiye Ambaye Alipasua mwangaza wa asubuhi kutoka kwenye giza la usiku, na Akaufanya usiku ni wakati wa utulivu, anatulia humo anayechoka mchana na kupata fungu lake la mapumziko, na Akalifanya jua na mwezi zinatembea katika njia zake kwa hesabu ya sawsawa iliyokadiriwa, haibadiliki wala haigongani. Hayo ndiyo makadirio ya Al- ’Azīz, Mwenye kushinda, ambaye ufalme Wake umeshinda, Al- ’Alīm, Aliye Mjuzi wa maslahi ya viumbe Wake na kuendesha mambo yao. Al- ’Azīz na Al- ’Alīm ni miongoni mwa majina ya Mwenyezi Mungu mazuri yanayoonesha ukamilifu wa ushindi na ujuzi
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek