Quran with Swahili translation - Surah Al-Mumtahanah ayat 7 - المُمتَحنَة - Page - Juz 28
﴿۞ عَسَى ٱللَّهُ أَن يَجۡعَلَ بَيۡنَكُمۡ وَبَيۡنَ ٱلَّذِينَ عَادَيۡتُم مِّنۡهُم مَّوَدَّةٗۚ وَٱللَّهُ قَدِيرٞۚ وَٱللَّهُ غَفُورٞ رَّحِيمٞ ﴾
[المُمتَحنَة: 7]
﴿عسى الله أن يجعل بينكم وبين الذين عاديتم منهم مودة والله قدير﴾ [المُمتَحنَة: 7]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Huenda Mwenyezi Mungu Akaweka baina yenu nyinyi, enyi Waumini, na wale jamaa zenu washirikina, ambao mlikuwa na uadui nao, mapenzi baada ya machukivu na maelewano baada ya ugomvi kwa kuvifanya vifua vyao viukunjukie Uislamu. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu, na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa msamaha kwa waja Wake ni Mwingi wa huruma Kwao |