Quran with Swahili translation - Surah Al-Mumtahanah ayat 6 - المُمتَحنَة - Page - Juz 28
﴿لَقَدۡ كَانَ لَكُمۡ فِيهِمۡ أُسۡوَةٌ حَسَنَةٞ لِّمَن كَانَ يَرۡجُواْ ٱللَّهَ وَٱلۡيَوۡمَ ٱلۡأٓخِرَۚ وَمَن يَتَوَلَّ فَإِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلۡغَنِيُّ ٱلۡحَمِيدُ ﴾
[المُمتَحنَة: 6]
﴿لقد كان لكم فيهم أسوة حسنة لمن كان يرجو الله واليوم الآخر﴾ [المُمتَحنَة: 6]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kwa hakika mlikuwa, enyi Waumini, na kiigizo chema kwa Ibrāhīm, amani imshukie, na wale waliokuwa na yeye, kwa anayetumai kupata kheri kutoka kwa Mwenyezi Mungu duniani na Akhera. Na yoyote anayeyapuuza yale ambayo Mwenyezi Mungu Anamuitia nayo ya kuwaiga Manabii Wake na akafanya urafiki na maadui Wake, basi Mwenyezi Mungu Ndiye Mkwasi wa kutowahitajia waja Wake, Ndiye Mwenye kuhimidiwa kwa dhati Yake na sifa Zake, Ndiye Mwenye kushukuriwa kwa namna zote |