Quran with Swahili translation - Surah As-saff ayat 13 - الصَّف - Page - Juz 28
﴿وَأُخۡرَىٰ تُحِبُّونَهَاۖ نَصۡرٞ مِّنَ ٱللَّهِ وَفَتۡحٞ قَرِيبٞۗ وَبَشِّرِ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ ﴾
[الصَّف: 13]
﴿وأخرى تحبونها نصر من الله وفتح قريب وبشر المؤمنين﴾ [الصَّف: 13]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na kuna neema nyingine kwenu, enyi Waumini, mtaipenda, nayo ni msaada kutoka kwa mwenyezi Mungu utakaowajia na ushindi wa haraka utakaopatikana mikononi mwenu. Na wape bishara Waumini, ewe Mtume, ya kunusuriwa na kupata ushindi duniani na kupata Pepo kesho Akhera |