Quran with Swahili translation - Surah As-saff ayat 14 - الصَّف - Page - Juz 28
﴿يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ كُونُوٓاْ أَنصَارَ ٱللَّهِ كَمَا قَالَ عِيسَى ٱبۡنُ مَرۡيَمَ لِلۡحَوَارِيِّـۧنَ مَنۡ أَنصَارِيٓ إِلَى ٱللَّهِۖ قَالَ ٱلۡحَوَارِيُّونَ نَحۡنُ أَنصَارُ ٱللَّهِۖ فَـَٔامَنَت طَّآئِفَةٞ مِّنۢ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ وَكَفَرَت طَّآئِفَةٞۖ فَأَيَّدۡنَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ عَلَىٰ عَدُوِّهِمۡ فَأَصۡبَحُواْ ظَٰهِرِينَ ﴾
[الصَّف: 14]
﴿ياأيها الذين آمنوا كونوا أنصار الله كما قال عيسى ابن مريم للحواريين﴾ [الصَّف: 14]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkafuata sheria Zake kivitendo! Kuweni watetezi wa dini ya Mwenyezi Mungu kama walivyokuwa marafiki wa kidhati wa ‘Īsā watetezi wa Dini ya Mwenyezi Mungu alipowaambia wao Īsā, «Ni nani atakayesimama kunihami na kunisaidia katika mambo ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu?» Wakasema, «Sisi ndio watetezi wa Dini ya Mwenyezi Mungu.» Hapo kundi moja la Wana wa Isrāīl likaongoka na kundi lingine likapotea, tukawapa nguvu wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na tukawapa ushindi juu ya wale waliowafanyia uadui miongoni mwa vipote vya Wanaswara, wakawa na nguvu juu yao kwa kutumilizwa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie |