Quran with Swahili translation - Surah Al-Munafiqun ayat 4 - المُنَافِقُونَ - Page - Juz 28
﴿۞ وَإِذَا رَأَيۡتَهُمۡ تُعۡجِبُكَ أَجۡسَامُهُمۡۖ وَإِن يَقُولُواْ تَسۡمَعۡ لِقَوۡلِهِمۡۖ كَأَنَّهُمۡ خُشُبٞ مُّسَنَّدَةٞۖ يَحۡسَبُونَ كُلَّ صَيۡحَةٍ عَلَيۡهِمۡۚ هُمُ ٱلۡعَدُوُّ فَٱحۡذَرۡهُمۡۚ قَٰتَلَهُمُ ٱللَّهُۖ أَنَّىٰ يُؤۡفَكُونَ ﴾
[المُنَافِقُونَ: 4]
﴿وإذا رأيتهم تعجبك أجسامهم وإن يقولوا تسمع لقولهم كأنهم خشب مسندة يحسبون﴾ [المُنَافِقُونَ: 4]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na unapowatazama wanafiki hawa, yanakufurahisha maumbile yao na mandhari yao, na wanapozungumza unayasikiliza mazungumzo yao kwa ufasaha wa ndimi zao, na hali wao kutokamana na utupu wa nyoyo zao kuwa hazina Imani na akili zao kuwa hazina fahamu wala elimu yenye manufaa, ni kama vigogo vilivyotegemezwa kwenye ukuta, visivyokuwa na uhai.wanadhania kila sauti ya ukelele inawashukia wao na ina madhara kwao kwa kujua kwao uhakika wa hali yao na uoga wao mwingi na hofu iliyojikita nyoyoni mwao. Wao ndio maadui wa kikwelikweli wenye uadui mwingi kwako wewe na kwa Waumini. Basi jichunge na wao, Mwenyezi Mungu Amewadhalilisha wao na Amewatoa kwenye rehema Yake. Basi ni vipi wao wanaiepuka haki na wanaelekea kwenye yale ambayo wao wamo ndani yake ya unafiki na upotevu |