Quran with Swahili translation - Surah Al-Munafiqun ayat 5 - المُنَافِقُونَ - Page - Juz 28
﴿وَإِذَا قِيلَ لَهُمۡ تَعَالَوۡاْ يَسۡتَغۡفِرۡ لَكُمۡ رَسُولُ ٱللَّهِ لَوَّوۡاْ رُءُوسَهُمۡ وَرَأَيۡتَهُمۡ يَصُدُّونَ وَهُم مُّسۡتَكۡبِرُونَ ﴾
[المُنَافِقُونَ: 5]
﴿وإذا قيل لهم تعالوا يستغفر لكم رسول الله لووا رءوسهم ورأيتهم يصدون﴾ [المُنَافِقُونَ: 5]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na wanapoambiwa hawa wanafiki, «Njooni huku hali ya kutubia mtake udhuru wa hayo yaliyotokea kwenu ya maneno maovu na mazungumzo ya ufidhuli, ili Mtume wa Mwenyezi Mungu awaombee Mwenyezi Mungu msamaha wa dhambi zenu , huvigeuza vichwa vyao na wakavitikisa kwa njia ya shere na kiburi. Na utawaona, ewe Mtume, wanakupa mgongo na huku wao wanalifanyia kiburi jambo la kufuata yale ambayo walitakiwa wayafuate |