Quran with Swahili translation - Surah AT-Talaq ayat 7 - الطَّلَاق - Page - Juz 28
﴿لِيُنفِقۡ ذُو سَعَةٖ مِّن سَعَتِهِۦۖ وَمَن قُدِرَ عَلَيۡهِ رِزۡقُهُۥ فَلۡيُنفِقۡ مِمَّآ ءَاتَىٰهُ ٱللَّهُۚ لَا يُكَلِّفُ ٱللَّهُ نَفۡسًا إِلَّا مَآ ءَاتَىٰهَاۚ سَيَجۡعَلُ ٱللَّهُ بَعۡدَ عُسۡرٖ يُسۡرٗا ﴾
[الطَّلَاق: 7]
﴿لينفق ذو سعة من سعته ومن قدر عليه رزقه فلينفق مما آتاه﴾ [الطَّلَاق: 7]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na atoe matumizi mume kulingana na kile alichokunjuliwa nacho na Mwenyezi Mungu kumpa mkewe aliyeachana naye na amlipie mwanawe, iwapo mume ana ukunjufu wa mapato. Na yule ambaye amebanika kimatumizi naye ni fukara, basi na atoe kulingana na kile alichopewa na Mwenyezi Mungu katika matumizi. Masikini halazimishwi kutoa kama kile anacholazimishwa tajiri. Mwenyezi Mungu Ataleta, baada ya dhiki na shida, ukunjufu wa maisha na kutosheka |