Quran with Swahili translation - Surah AT-Talaq ayat 6 - الطَّلَاق - Page - Juz 28
﴿أَسۡكِنُوهُنَّ مِنۡ حَيۡثُ سَكَنتُم مِّن وُجۡدِكُمۡ وَلَا تُضَآرُّوهُنَّ لِتُضَيِّقُواْ عَلَيۡهِنَّۚ وَإِن كُنَّ أُوْلَٰتِ حَمۡلٖ فَأَنفِقُواْ عَلَيۡهِنَّ حَتَّىٰ يَضَعۡنَ حَمۡلَهُنَّۚ فَإِنۡ أَرۡضَعۡنَ لَكُمۡ فَـَٔاتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ وَأۡتَمِرُواْ بَيۡنَكُم بِمَعۡرُوفٖۖ وَإِن تَعَاسَرۡتُمۡ فَسَتُرۡضِعُ لَهُۥٓ أُخۡرَىٰ ﴾
[الطَّلَاق: 6]
﴿أسكنوهن من حيث سكنتم من وجدكم ولا تضاروهن لتضيقوا عليهن وإن كن﴾ [الطَّلَاق: 6]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Wakalisheni, wale walioachwa miongoni mwa wake zenu kwenye kipindi chao eda, mahali mfano wa pale mnapokaa nyinyi kwa kadiri ya ukunjufu wenu na uwezo wenu. Wala msiwafanyie mambo ya kuwadhuru mkawatilia mkazo katika makazi. Na iwapo wake zenu waliopewa talaka ni waja wazito, basi wapeni matumizi pindi wakiwa kwenye eda lao mpaka watakapozaa. Na iwapo watawanyonyeshea nyinyi watoto wao ambao ni wenu kwa malipo, basi wapeni malipo yao, na amrishaneni nyinyi kwa nyinyi wema na roho nzuri. Na iwapo hamkukubaliana juu ya unyonyeshaji wa mama mzazi, basi baba atanyonyeshewa na mnyonyeshaji mwingine asiyekuwa mama aliyepewa talaka |