×

Mwenyezi Mungu amewapigia mfano walio kufuru: mke wa Nuhu na mke wa 66:10 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah At-Tahrim ⮕ (66:10) ayat 10 in Swahili

66:10 Surah At-Tahrim ayat 10 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah At-Tahrim ayat 10 - التَّحرِيم - Page - Juz 28

﴿ضَرَبَ ٱللَّهُ مَثَلٗا لِّلَّذِينَ كَفَرُواْ ٱمۡرَأَتَ نُوحٖ وَٱمۡرَأَتَ لُوطٖۖ كَانَتَا تَحۡتَ عَبۡدَيۡنِ مِنۡ عِبَادِنَا صَٰلِحَيۡنِ فَخَانَتَاهُمَا فَلَمۡ يُغۡنِيَا عَنۡهُمَا مِنَ ٱللَّهِ شَيۡـٔٗا وَقِيلَ ٱدۡخُلَا ٱلنَّارَ مَعَ ٱلدَّٰخِلِينَ ﴾
[التَّحرِيم: 10]

Mwenyezi Mungu amewapigia mfano walio kufuru: mke wa Nuhu na mke wa Lut'i. Walikuwa chini ya waja wetu wema wawili miongoni mwa waja wetu. Lakini wakawakhuni waume zao, nao wasiwafae kitu. Na ikasemwa: Ingieni Motoni pamoja na wanao ingia

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ضرب الله مثلا للذين كفروا امرأة نوح وامرأة لوط كانتا تحت عبدين, باللغة السواحيلية

﴿ضرب الله مثلا للذين كفروا امرأة نوح وامرأة لوط كانتا تحت عبدين﴾ [التَّحرِيم: 10]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Mwenyezi Mungu Anapiga mfano wa hali ya makafiri- katika kutangamana kwao na Waislamu, kuwa karibu na wao na kutangamana nao na kwamba hilo halitawanufaisha kwa kuwa wamemkufuru Mwenyezi Mungu- kuwa ni kama hali ya mke wa Nabii wa Mwenyezi Mungu, Nūḥ, na mke wa Nabii wa Mwenyezi mungu, Lūṭ, kwa kuwa wote wawili walikuwa chini ya hifadhi ya ndoa ya waja wawili wema miongoni mwa waja wetu, ukapatikana kutoka kwao kuwafanyia uhaini wa kidini, kwani wote wawili walikuwa makafiri. Mitume wawili hawa hawakuweza kuwatetea wake zao na adhabu ya Mwenyezi Mungu, na wakaambiwa wake wawili hao, «Ingieni Motoni pamoja na wenye kuingia huko.» Katika kupiga mfano huu pana dalili ya kwamba kuwa karibu na Manabii na watu wema hakufai kitu iwapo mtu mwenyewe ana matendo mabaya
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek