Quran with Swahili translation - Surah At-Tahrim ayat 11 - التَّحرِيم - Page - Juz 28
﴿وَضَرَبَ ٱللَّهُ مَثَلٗا لِّلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱمۡرَأَتَ فِرۡعَوۡنَ إِذۡ قَالَتۡ رَبِّ ٱبۡنِ لِي عِندَكَ بَيۡتٗا فِي ٱلۡجَنَّةِ وَنَجِّنِي مِن فِرۡعَوۡنَ وَعَمَلِهِۦ وَنَجِّنِي مِنَ ٱلۡقَوۡمِ ٱلظَّٰلِمِينَ ﴾
[التَّحرِيم: 11]
﴿وضرب الله مثلا للذين آمنوا امرأة فرعون إذ قالت رب ابن لي﴾ [التَّحرِيم: 11]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na Mwenyezi Mungu Anapiga mfano wa hali ya Waumini- waliomuamini Mwenyezi Munmgu, wakamuabudu Peke Yake na wakazifuata Sheria Zake kivitendo na kwamba wao hakuwadhuru wao kule kutangamana kwao na makfiri katika maingilaiano yao- kuwa ni kama hali ya mke wa Fir'awn aliyekuwa kwenye hifadhi ya ndoa ya aliyekuwa muovu mno miongoni mwa wale waliomkufuru Mwenyezi Mungu, na hali yeye alikuwa anamuamini Mwenyezi Mungu, pindi aliposema, «Mola wangu! Nijengee Nyumba huko kwako Peponi na uniokoe na utawala wa Fir'awn na ukafiri wake na yale matendo maovu yanayotokana na yeye, Na uniokoe na watu wenye kumfuata katika udhalimu na upotevu, na uniokoe na mateso yao |