Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 134 - الأعرَاف - Page - Juz 9
﴿وَلَمَّا وَقَعَ عَلَيۡهِمُ ٱلرِّجۡزُ قَالُواْ يَٰمُوسَى ٱدۡعُ لَنَا رَبَّكَ بِمَا عَهِدَ عِندَكَۖ لَئِن كَشَفۡتَ عَنَّا ٱلرِّجۡزَ لَنُؤۡمِنَنَّ لَكَ وَلَنُرۡسِلَنَّ مَعَكَ بَنِيٓ إِسۡرَٰٓءِيلَ ﴾
[الأعرَاف: 134]
﴿ولما وقع عليهم الرجز قالوا ياموسى ادع لنا ربك بما عهد عندك﴾ [الأعرَاف: 134]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na adhabu ilipomteremkia Fir'awn na watu wake, walimkimbilia Mūsā na wakasema, «Ewe Mūsā, tuombee Mola wako, kwa wahyi aliokuletea Mwenyezi Mungu kwamba adhabu huondolewa kwa kutubia. Na ukituondolea adhabu tuliyonayo, tutayaamini uliyokuja nayo, na tutayafuata uliyotuitia kwayo, na tutawaachilia, pamoja na wewe, Wana wa Isrāīl, hatutawazuia waende na wewe pale wanapotaka |