Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 158 - الأعرَاف - Page - Juz 9
﴿قُلۡ يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ إِنِّي رَسُولُ ٱللَّهِ إِلَيۡكُمۡ جَمِيعًا ٱلَّذِي لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِۖ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ يُحۡيِۦ وَيُمِيتُۖ فَـَٔامِنُواْ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِ ٱلنَّبِيِّ ٱلۡأُمِّيِّ ٱلَّذِي يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ وَكَلِمَٰتِهِۦ وَٱتَّبِعُوهُ لَعَلَّكُمۡ تَهۡتَدُونَ ﴾
[الأعرَاف: 158]
﴿قل ياأيها الناس إني رسول الله إليكم جميعا الذي له ملك السموات﴾ [الأعرَاف: 158]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Waambie, ewe Mtume, watu wote, «Mimi ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu kwenu nyote, si kwa baadhi yenu bila ya wengine, Ambaye ni wake ufalme wa mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake. Haifai kuelekezwa uungu na ibada isipokuwa Kwake, zilizotukuka sifa Zake, Mwenye uwezo wa kupatisha viumbe, kuwaondosha na kuwafufua. Basi muaminini Mwenyezi Mungu na kubalini upweke Wake, na muaminini Mtume Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani imshukiye, Nabii asiyesoma wala kwandika, anayemuamini Mwenyezi Mungu na yale aliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wake na yale waliyoteremshiwa manabii kabla yake; Mfuateni Mtume huyu na jilazimisheni kuyafanya anayowaamrisha kwayo ya kumtii Mwenyezi Mungu kwa kutaraji muafikiwe kufuata njia iliyolingana sawa.» |