×

Na tuliwagawanya katika makabila kumi na mbili, mataifa mbali mbali. Na tulimfunulia 7:160 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-A‘raf ⮕ (7:160) ayat 160 in Swahili

7:160 Surah Al-A‘raf ayat 160 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 160 - الأعرَاف - Page - Juz 9

﴿وَقَطَّعۡنَٰهُمُ ٱثۡنَتَيۡ عَشۡرَةَ أَسۡبَاطًا أُمَمٗاۚ وَأَوۡحَيۡنَآ إِلَىٰ مُوسَىٰٓ إِذِ ٱسۡتَسۡقَىٰهُ قَوۡمُهُۥٓ أَنِ ٱضۡرِب بِّعَصَاكَ ٱلۡحَجَرَۖ فَٱنۢبَجَسَتۡ مِنۡهُ ٱثۡنَتَا عَشۡرَةَ عَيۡنٗاۖ قَدۡ عَلِمَ كُلُّ أُنَاسٖ مَّشۡرَبَهُمۡۚ وَظَلَّلۡنَا عَلَيۡهِمُ ٱلۡغَمَٰمَ وَأَنزَلۡنَا عَلَيۡهِمُ ٱلۡمَنَّ وَٱلسَّلۡوَىٰۖ كُلُواْ مِن طَيِّبَٰتِ مَا رَزَقۡنَٰكُمۡۚ وَمَا ظَلَمُونَا وَلَٰكِن كَانُوٓاْ أَنفُسَهُمۡ يَظۡلِمُونَ ﴾
[الأعرَاف: 160]

Na tuliwagawanya katika makabila kumi na mbili, mataifa mbali mbali. Na tulimfunulia Musa walipo muomba maji watu wake kumwambia: Lipige hilo jiwe kwa fimbo yako. Mara zikatibuka humo chemchem kumi na mbili, na kila watu wakajua mahali pao pa kunywea. Na tukawafunika kivuli kwa mawingu, na tukawateremshia Manna na Salwa. Tukawaambia: Kuleni vizuri hivi tulivyo kuruzukuni. Wala hawakutu- dhulumu Sisi, bali wamejidhulumu wenyewe

❮ Previous Next ❯

ترجمة: وقطعناهم اثنتي عشرة أسباطا أمما وأوحينا إلى موسى إذ استسقاه قومه أن, باللغة السواحيلية

﴿وقطعناهم اثنتي عشرة أسباطا أمما وأوحينا إلى موسى إذ استسقاه قومه أن﴾ [الأعرَاف: 160]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na tuliwagawa watu wa Mūsā miongoni mwa Wana wa Isrāīl makabila kumi na mbili, kwa idadi ya Asbāṭ- wana wa Ya’qūb-, kila kabila ikajulikana kupitia kiongozi wake. Na tulimpelekea wahyi Mūsā, walipotaka watu wake kwake maji ya kunywa waliposhikwa na kiu katika kuzunguka kwao, tukamwambia, «Lipige hilo jiwe kwa fimbo yako.» Akalipiga na pakabubujika chemchemi za maji sehemu kumi na mbili, na watu wa kila kabila, miongoni mwa yale makabila kumi na mbili, walijua mahali pao pa kunywa, hakuna kabila litakaloingia sehemu ya kunywa ya kabila lingine. Na tukawafinika kiwingu juu yenu, na tukawateremshia mann- kitu kinachofanana na gundi chenye ladha kama ya asali- na salwā- ndege wanaofanana na wale wanaoitwa sumānā (tomboro), na tukawaambia, «Kuleni vitu vizuri tulivyowaruzuku.» Walivichukia na kuvichoka hivyo kwa muda mrefu wa kuvitumia na wakasema, «Hatutavumilia juu ya chakula kimoja.» Na wakataka kubadilishiwa kizuri walichonacho kwa ambacho ni kiovu. Na wao hawakutudhulumu sisi walipoacha kumshukuru Mwenyezi Mungu na kuacha kusimama na yale Aliyoyalazimisha Mwenyezi Mungu juu yao, lakini walikuwa wakizidhulumu nafsi zao, kwa kuwa walizikosesha kila jema na kuzipeleka kwenye shari na mateso
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek