Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 161 - الأعرَاف - Page - Juz 9
﴿وَإِذۡ قِيلَ لَهُمُ ٱسۡكُنُواْ هَٰذِهِ ٱلۡقَرۡيَةَ وَكُلُواْ مِنۡهَا حَيۡثُ شِئۡتُمۡ وَقُولُواْ حِطَّةٞ وَٱدۡخُلُواْ ٱلۡبَابَ سُجَّدٗا نَّغۡفِرۡ لَكُمۡ خَطِيٓـَٰٔتِكُمۡۚ سَنَزِيدُ ٱلۡمُحۡسِنِينَ ﴾
[الأعرَاف: 161]
﴿وإذ قيل لهم اسكنوا هذه القرية وكلوا منها حيث شئتم وقولوا حطة﴾ [الأعرَاف: 161]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na kumbuka, ewe Mtume, uasi kwa Wana wa Isrāīl Mola wao, kutakata na sifa pungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, na Nabii wao Mūsā, amani imshukiye, na kugeuza kwao maneno waliyoamrishwa wayaseme pindi Alipowaambia Mwenyezi Mungu, «kaeni mji wa Baitul Maqdis na kuleni matunda yake, nafaka zake na mimea yake popote mtakapo na wakati wowote mtakao na semeni, ‘tuondoshee dhambi zetu,’ na ingieni mlangoni mkimnyenyekea Mwenyezi Mungu, tutawasamehe makosa yenu na hatutawaadhibu kwayo, na tutawaongezea walio wema kheri mbili: za ulimwengu na Akhera |