Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 168 - الأعرَاف - Page - Juz 9
﴿وَقَطَّعۡنَٰهُمۡ فِي ٱلۡأَرۡضِ أُمَمٗاۖ مِّنۡهُمُ ٱلصَّٰلِحُونَ وَمِنۡهُمۡ دُونَ ذَٰلِكَۖ وَبَلَوۡنَٰهُم بِٱلۡحَسَنَٰتِ وَٱلسَّيِّـَٔاتِ لَعَلَّهُمۡ يَرۡجِعُونَ ﴾
[الأعرَاف: 168]
﴿وقطعناهم في الأرض أمما منهم الصالحون ومنهم دون ذلك وبلوناهم بالحسنات والسيئات﴾ [الأعرَاف: 168]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na tuliwagawanya Wana wa Isrāīl makundi: kati yao kuna wanaosimama kutekeleza haki za Mwenyezi Mungu na haki za waja Wake, na kati yao kuna wenye kufanya kasoro wenye kuzidhulumu nafsi zao. Na hawa tuliwapa mtihani wa maisha ya neema na ukunjufu wa riziki; na pia tuliwapa mtihani wa maisha ya dhiki, misiba na matatizo kwa matarajio kuwa watarudi kumtii Mola wao na watatubia kutokana na vitendo vya kumuasi |