×

Na wakafuatia baada yao kizazi kibaya walio rithi Kitabu. Wakashika anasa za 7:169 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-A‘raf ⮕ (7:169) ayat 169 in Swahili

7:169 Surah Al-A‘raf ayat 169 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 169 - الأعرَاف - Page - Juz 9

﴿فَخَلَفَ مِنۢ بَعۡدِهِمۡ خَلۡفٞ وَرِثُواْ ٱلۡكِتَٰبَ يَأۡخُذُونَ عَرَضَ هَٰذَا ٱلۡأَدۡنَىٰ وَيَقُولُونَ سَيُغۡفَرُ لَنَا وَإِن يَأۡتِهِمۡ عَرَضٞ مِّثۡلُهُۥ يَأۡخُذُوهُۚ أَلَمۡ يُؤۡخَذۡ عَلَيۡهِم مِّيثَٰقُ ٱلۡكِتَٰبِ أَن لَّا يَقُولُواْ عَلَى ٱللَّهِ إِلَّا ٱلۡحَقَّ وَدَرَسُواْ مَا فِيهِۗ وَٱلدَّارُ ٱلۡأٓخِرَةُ خَيۡرٞ لِّلَّذِينَ يَتَّقُونَۚ أَفَلَا تَعۡقِلُونَ ﴾
[الأعرَاف: 169]

Na wakafuatia baada yao kizazi kibaya walio rithi Kitabu. Wakashika anasa za haya maisha duni, na wakasema: Tutasamehewa! Na ikiwajia tena anasa kama hiyo wataishika pia. Je, hawakufanyiwa agano la Kitabu kuwa wasiseme juu ya Mwenyezi Mungu ila Haki tu? Nao wamekwisha soma yaliomo humo. Na nyumba ya Akhera ni bora kwa wanao jikinga na maasi. Basi je, hamtii akilini

❮ Previous Next ❯

ترجمة: فخلف من بعدهم خلف ورثوا الكتاب يأخذون عرض هذا الأدنى ويقولون سيغفر, باللغة السواحيلية

﴿فخلف من بعدهم خلف ورثوا الكتاب يأخذون عرض هذا الأدنى ويقولون سيغفر﴾ [الأعرَاف: 169]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Wakaja, baada ya hawa ambao tulieleza sifa zao, badala mbovu. Walichukua Kitabu kutoka kwa wakale wao, wakakisoma na wakakijua, na wakaenda kinyume na hukumu zake, wakawa wanachukua kile wanacholetewa cha starahe ya ulimwenguni kinachotokana na njia mbaya za mapato kama hongo na mfano wake. Hayo ni kwa sababu ya wingi wa pupa lao na uroho wao, na wanasema pamoja na hayo, «Mwenyezi Mungu Atatusamehe,» wakitamani kwa Mwenyezi Mungu mambo yasiyofaa, na ikiwajia Mayahudi hawa starahe yenye kuondoka, miongoni mwa vitu vya haramu, huichukua na kuihalalisha, huku wakiendelea kufanya madhambi yao na kutumia haramu. Kwani hazikuchukuliwa kwao ahadi juu ya kuisimamisha Taurati na kufuata kivitendo yaliyomo ndani yake na kwamba hawatasema juu ya Mwenyezi Mungu isipokuwa ukweli na kwamba hawatamzulia urongo, wakayajua yaliyomo Kitabuni, wakayapoteza na wakaenda kinyume na ahadi ya Mwenyezi Mungu kwao katika hilo? Na nyumba ya Akhera ni bora zaidi kwa wanaomcha Mwenyezi Mungu, wakafuata amri Zake na wakaepuka makatazo Yake. Kwani hawa wanaochukua mapato duni hawaelewi kwamba yaliyo mbele ya Mwenyezi Mungu ni bora zaidi na yenye kusalia zaidi kwa wachamungu
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek