×

Na tumeiumbia Jahannamu majini wengi na watu. Wana nyoyo, lakini hawafahamu kwazo. 7:179 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-A‘raf ⮕ (7:179) ayat 179 in Swahili

7:179 Surah Al-A‘raf ayat 179 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 179 - الأعرَاف - Page - Juz 9

﴿وَلَقَدۡ ذَرَأۡنَا لِجَهَنَّمَ كَثِيرٗا مِّنَ ٱلۡجِنِّ وَٱلۡإِنسِۖ لَهُمۡ قُلُوبٞ لَّا يَفۡقَهُونَ بِهَا وَلَهُمۡ أَعۡيُنٞ لَّا يُبۡصِرُونَ بِهَا وَلَهُمۡ ءَاذَانٞ لَّا يَسۡمَعُونَ بِهَآۚ أُوْلَٰٓئِكَ كَٱلۡأَنۡعَٰمِ بَلۡ هُمۡ أَضَلُّۚ أُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلۡغَٰفِلُونَ ﴾
[الأعرَاف: 179]

Na tumeiumbia Jahannamu majini wengi na watu. Wana nyoyo, lakini hawafahamu kwazo. Na wana macho, lakini hawaoni kwayo. Na wana masikio, lakini hawasikii kwayo. Hao ni kama nyama howa, bali wao ni wapotofu zaidi. Hao ndio walio ghafilika

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ولقد ذرأنا لجهنم كثيرا من الجن والإنس لهم قلوب لا يفقهون بها, باللغة السواحيلية

﴿ولقد ذرأنا لجهنم كثيرا من الجن والإنس لهم قلوب لا يفقهون بها﴾ [الأعرَاف: 179]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na kwa hakika tuliuumbia Moto - ambao ndani yake Mwenyezi Mungu Atawaadhibu wanaostahili kuadhibiwa huko Akhera- majini na binadamu wengi, wana nyoyo lakini hawaelewi kwazo, hawatazamii malipo mazuri wala hawaogopi mateso; na wana macho hawaangalii kwayo aya za Mwenyezi Mungu na dalili Zake, na wana masikio hawasikii kwayo aya za Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kuzitia akilini. Hawa ni kama wanyama wasioelewa waambiwacho, wasiofahamu wakionacho na wasiotia akilini kwa nyoyo zao kizuri na kibaya wakaweza kuzitenganisha. Bali wao wamepotea zaidi kuliko hao wanyama, kwani wanyama wanaona yanayowafaa na yanayowadhuru na wanamfuata mchungaji wao. Ama wao ni kinyume cha hilo, wao ndio wenye kughafilika na jambo la kumuamini Mwenyezi Mungu na kumtii
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek