Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 180 - الأعرَاف - Page - Juz 9
﴿وَلِلَّهِ ٱلۡأَسۡمَآءُ ٱلۡحُسۡنَىٰ فَٱدۡعُوهُ بِهَاۖ وَذَرُواْ ٱلَّذِينَ يُلۡحِدُونَ فِيٓ أَسۡمَٰٓئِهِۦۚ سَيُجۡزَوۡنَ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ ﴾
[الأعرَاف: 180]
﴿ولله الأسماء الحسنى فادعوه بها وذروا الذين يلحدون في أسمائه سيجزون ما﴾ [الأعرَاف: 180]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na Mwenyezi Mungu, kutakata na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake, Ana Majina Mazuri yanayoonyesha ukamilifu wa uwezo Wake, na majina Yake yote ni mazuri. Basi ombeni kutoka Kwake, kwa majina Yake, mnachotaka na muwaacheni wale wanaogeuza majina Yake kwa kuzidisha na kupunguza au kupotoa, kama kumuita kwa majina hayo asiyeyastahiki, kama vile washirikina wanavyowaita, kwa majina hayo, waungu wao, au ayape majina hayo maana ambayo Mwenyezi Mungu Hakuyataka wala Mtume Wake. Basi watapata malipo ya matendo yao mabaya waliokuwa wakiyafanya ulimwenguni ya kumkanusha Mwenyezi Mungu, kuyapotoa majina Yake na kuwafanya warongo Mitume Wake |