Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 182 - الأعرَاف - Page - Juz 9
﴿وَٱلَّذِينَ كَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَا سَنَسۡتَدۡرِجُهُم مِّنۡ حَيۡثُ لَا يَعۡلَمُونَ ﴾
[الأعرَاف: 182]
﴿والذين كذبوا بآياتنا سنستدرجهم من حيث لا يعلمون﴾ [الأعرَاف: 182]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na wale ambao walizikanusha aya zetu wakazikataa na wasiwaidhike nazo, tutawafungulia milango ya riziki na njia za maisha katika ulimwengu, kwa kuwavuta kidogo kidogo mpaka wahadaike kwa yale ambayo wako nayo na waitakidi kuwa wao wako kwenye kitu cha maana, kisha tutawatesa kwa ghafla kwa namna wasioijua. Haya ni mateso yatokao kwa Mwenyezi Mungu ya kukanusha hoja za Mwenyezi Mungu na aya Zake |