Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 194 - الأعرَاف - Page - Juz 9
﴿إِنَّ ٱلَّذِينَ تَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ عِبَادٌ أَمۡثَالُكُمۡۖ فَٱدۡعُوهُمۡ فَلۡيَسۡتَجِيبُواْ لَكُمۡ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ ﴾
[الأعرَاف: 194]
﴿إن الذين تدعون من دون الله عباد أمثالكم فادعوهم فليستجيبوا لكم إن﴾ [الأعرَاف: 194]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kwa hakika wale ambao mnawaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, enyi washirikina, wamemilikiwa na Mola wao, kama mlivyomilikiwa nyinyi na Mola wenu. Basi iwapo nyinyi, kama mnavyodai, ni wakweli kwamba wao wanastahiki wafayiwe chochote kile cha ibada, waiteni wawaitikie. Iwapo watawaitikia na watawapatia matakwa yenu, mtakuwa ni wakweli, na isipokuwa hivyo, itakuwa wazi kwamba nyinyi ni warongo mnamzulia Mwenyezi Mungu uzushi mkubwa kabisa |