×

Je, wao wanayo miguu ya kwendea? Au wanayo mikono ya kutetea? Au 7:195 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-A‘raf ⮕ (7:195) ayat 195 in Swahili

7:195 Surah Al-A‘raf ayat 195 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 195 - الأعرَاف - Page - Juz 9

﴿أَلَهُمۡ أَرۡجُلٞ يَمۡشُونَ بِهَآۖ أَمۡ لَهُمۡ أَيۡدٖ يَبۡطِشُونَ بِهَآۖ أَمۡ لَهُمۡ أَعۡيُنٞ يُبۡصِرُونَ بِهَآۖ أَمۡ لَهُمۡ ءَاذَانٞ يَسۡمَعُونَ بِهَاۗ قُلِ ٱدۡعُواْ شُرَكَآءَكُمۡ ثُمَّ كِيدُونِ فَلَا تُنظِرُونِ ﴾
[الأعرَاف: 195]

Je, wao wanayo miguu ya kwendea? Au wanayo mikono ya kutetea? Au wanayo macho ya kuonea? Au wanayo masikio ya kusikizia? Sema: Iiteni hio miungu yenu ya ushirikina. Kisha nifanyieni mimi vitimbi, wala msinipe muhula

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ألهم أرجل يمشون بها أم لهم أيد يبطشون بها أم لهم أعين, باللغة السواحيلية

﴿ألهم أرجل يمشون بها أم لهم أيد يبطشون بها أم لهم أعين﴾ [الأعرَاف: 195]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Je, waungu hawa na masanamu wana miguu ya kutembelea na nyinyi katika haja zenu? Au wao wana mikono ya kuwatetea na kuwanusuru juu ya anayewatakia shari na maovu? Au wao wana macho ya kutazamia, wakapata kuwajulisha yale waliyoyashuhudia na wakayaona miongoni mwa yale yaliyofichika kwenu mkawa hamuyaoni? Au wao wana masikio ya kusikia kwayo, wapate kuwapa habari ya yale msiyoyasikia? Iwapo waungu wenu ambao mnawaabudu hawana vyombo hivi, kuna maana gani kuwaabudu, ilhali wao hawana vitu hivi ambavyo kwavyo kunapelekea kujipatia manufaa au kujiepushia madhara? Waambie, ewe Mtume, kuwaambia hawa washirikina wenye kuwaabudu masanamu, «Waiteni waungu wenu ambao mliwafanya ni washirika wa Mwenyezi Mungu katika ibada, kisha kusanyikeni kunifanyia ubaya na maudhi, msinipe muhula na lifanyieni haraka hilo, kwani mimi siwajali waungu wenu kwa kuwa nategemea hifadhi ya Mwenyezi Mungu Peke Yake
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek