Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 203 - الأعرَاف - Page - Juz 9
﴿وَإِذَا لَمۡ تَأۡتِهِم بِـَٔايَةٖ قَالُواْ لَوۡلَا ٱجۡتَبَيۡتَهَاۚ قُلۡ إِنَّمَآ أَتَّبِعُ مَا يُوحَىٰٓ إِلَيَّ مِن رَّبِّيۚ هَٰذَا بَصَآئِرُ مِن رَّبِّكُمۡ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٞ لِّقَوۡمٖ يُؤۡمِنُونَ ﴾
[الأعرَاف: 203]
﴿وإذا لم تأتهم بآية قالوا لولا اجتبيتها قل إنما أتبع ما يوحى﴾ [الأعرَاف: 203]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na usipowajia, ewe Mtume, washirikina hawa na aya wanasema, «Si uitunge na uizue wewe mwenyewe.» Waambie, ewe Mtume, «Hili si langu, na haifai kwangu mimi nilifanye. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu Ameniamuru kufuata wahyi nilioletewa kutoka Kwake. Nao ni hii Qur’ani ninayowasomea, inayokusanya hoja na dalili zinazotoka kwa Mola wenu na yenye ufafanuzi, inayoongoza Waumini kwenye njia iliyolingana sawa, na ni rehema ambayo kwayo Mwenyezi Mungu Anawarehemu waja Wake Waumini |