Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 202 - الأعرَاف - Page - Juz 9
﴿وَإِخۡوَٰنُهُمۡ يَمُدُّونَهُمۡ فِي ٱلۡغَيِّ ثُمَّ لَا يُقۡصِرُونَ ﴾
[الأعرَاف: 202]
﴿وإخوانهم يمدونهم في الغي ثم لا يقصرون﴾ [الأعرَاف: 202]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na ndugu wa mashetani, nao ni wapotofu miongoni mwa wapotevu wa wanadamu ambao mashetani wanawasukuma kwenye upotevu na upotofu. Na mashetani wa kijini hawaachi nafasi iwapite katika kuwasukuma kwao mashetani wa kibinadamu kwenye upotofu. Na mashetani wa kibinadamu hawaachi nafasi iwapite katika kuyafanya yale ambayo mashetani wa kijini wanayafanyia ushawishi |