×

Sema: Mola Mlezi wangu ameharimisha mambo machafu ya dhaahiri na ya siri, 7:33 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-A‘raf ⮕ (7:33) ayat 33 in Swahili

7:33 Surah Al-A‘raf ayat 33 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 33 - الأعرَاف - Page - Juz 8

﴿قُلۡ إِنَّمَا حَرَّمَ رَبِّيَ ٱلۡفَوَٰحِشَ مَا ظَهَرَ مِنۡهَا وَمَا بَطَنَ وَٱلۡإِثۡمَ وَٱلۡبَغۡيَ بِغَيۡرِ ٱلۡحَقِّ وَأَن تُشۡرِكُواْ بِٱللَّهِ مَا لَمۡ يُنَزِّلۡ بِهِۦ سُلۡطَٰنٗا وَأَن تَقُولُواْ عَلَى ٱللَّهِ مَا لَا تَعۡلَمُونَ ﴾
[الأعرَاف: 33]

Sema: Mola Mlezi wangu ameharimisha mambo machafu ya dhaahiri na ya siri, na dhambi, na uasi bila ya haki, na kumshirikisha Mwenyezi Mungu na asicho kiletea uthibitisho, na kumzulia Mwenyezi Mungu msiyo yajua

❮ Previous Next ❯

ترجمة: قل إنما حرم ربي الفواحش ما ظهر منها وما بطن والإثم والبغي, باللغة السواحيلية

﴿قل إنما حرم ربي الفواحش ما ظهر منها وما بطن والإثم والبغي﴾ [الأعرَاف: 33]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Sema,ewe Mtume, kuwaambia washirikina hawa, «Hakika Mwenyezi Mungu Ndiye Aliyeyafanya matendo maovu kuwa ni haramu, yale yaliyo waziwazi na yale yaliyofichika, na Ameyakataza maasia yote, na miongoni mwa makubwa zaidi ya maasia ni kuwafanyia watu uadui, kwani hilo liko kando na haki. Na Amewaharamishia kuabudu, pamoja na Mwenyezi Mungu, Aliyetuka, vitu vyingine kati ya vile ambavyo Hakuviteremshia ushahidi wala hoja, kwani afanyaye hayo hana kithibitisho chochote. Na Amewaharamishia kumnasibishia Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, sheria ambayo Hakuipasisha kwa kumzulia urongo,» kama madai ya kwamba Mwenyezi Mungu Ana mwana na kuharamisha baadhi ya vilivyo halali katika mavazi na chakula
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek