Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 37 - الأعرَاف - Page - Juz 8
﴿فَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّنِ ٱفۡتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا أَوۡ كَذَّبَ بِـَٔايَٰتِهِۦٓۚ أُوْلَٰٓئِكَ يَنَالُهُمۡ نَصِيبُهُم مِّنَ ٱلۡكِتَٰبِۖ حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءَتۡهُمۡ رُسُلُنَا يَتَوَفَّوۡنَهُمۡ قَالُوٓاْ أَيۡنَ مَا كُنتُمۡ تَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِۖ قَالُواْ ضَلُّواْ عَنَّا وَشَهِدُواْ عَلَىٰٓ أَنفُسِهِمۡ أَنَّهُمۡ كَانُواْ كَٰفِرِينَ ﴾
[الأعرَاف: 37]
﴿فمن أظلم ممن افترى على الله كذبا أو كذب بآياته أولئك ينالهم﴾ [الأعرَاف: 37]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakuna yoyote aliye na udhalimu zaidi kuliko yule anayemzulia Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, urongo au akazikanusha aya Zake zilizoteremshwa, hao itawafikia sehemu yao ya adhabu waliyoandikiwa katika Al-Lawh( Al-Mhfūd) (Ubao uliohifadhiwa) mpaka atakapowajia Malaika wa mauti pamoja na wasaidizi wake kuzichukua roho zao, watawaambia, «Wako wapi wale mliokuwa mnawaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, kati ya washirika, wategemewa na masanamu, waje wawaokoe na janga lililowafika?» Watasema, «Wametutoroka.» Wakati huo watakiri makosa kwamba wao duniani walikuwa ni wenye kuupinga na kuukanusha upweke wa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka |