Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 52 - الأعرَاف - Page - Juz 8
﴿وَلَقَدۡ جِئۡنَٰهُم بِكِتَٰبٖ فَصَّلۡنَٰهُ عَلَىٰ عِلۡمٍ هُدٗى وَرَحۡمَةٗ لِّقَوۡمٖ يُؤۡمِنُونَ ﴾
[الأعرَاف: 52]
﴿ولقد جئناهم بكتاب فصلناه على علم هدى ورحمة لقوم يؤمنون﴾ [الأعرَاف: 52]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakika tumewaletea makafiri Qur’ani tuliyokuteremshia wewe, ewe Mtume, tuliyoibainisha, inayokusanya elimu kubwa, yenye kuongoza, kutoa kwenye upotevu, kupeleka kwenye njia ya usawa, hali ya kuwa ni rehema kwa watu wanaomuamini Mwenyezi Mungu na kuzitumia sheria Zake. Amewahusu wenye kuamini kwa kuwataja, bila ya wengine, ni kwamba wao ndio wenye kunufaika nayo |