×

Na Yeye ndiye anaye peleka pepo (za kuvuma) kuwa ni bishara kabla 7:57 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-A‘raf ⮕ (7:57) ayat 57 in Swahili

7:57 Surah Al-A‘raf ayat 57 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 57 - الأعرَاف - Page - Juz 8

﴿وَهُوَ ٱلَّذِي يُرۡسِلُ ٱلرِّيَٰحَ بُشۡرَۢا بَيۡنَ يَدَيۡ رَحۡمَتِهِۦۖ حَتَّىٰٓ إِذَآ أَقَلَّتۡ سَحَابٗا ثِقَالٗا سُقۡنَٰهُ لِبَلَدٖ مَّيِّتٖ فَأَنزَلۡنَا بِهِ ٱلۡمَآءَ فَأَخۡرَجۡنَا بِهِۦ مِن كُلِّ ٱلثَّمَرَٰتِۚ كَذَٰلِكَ نُخۡرِجُ ٱلۡمَوۡتَىٰ لَعَلَّكُمۡ تَذَكَّرُونَ ﴾
[الأعرَاف: 57]

Na Yeye ndiye anaye peleka pepo (za kuvuma) kuwa ni bishara kabla ya kufika rehema yake. Hata hizo pepo zinapo beba mawingu mazito tunayachunga mpaka kwenye nchi iliyo kufa. Kisha tunateremsha kwayo maji, ndio kama hivyo tukatolesha kila aina ya matunda. Basi hali kadhaalika tunavyo wafufua wafu, ili mpate kukumbuka

❮ Previous Next ❯

ترجمة: وهو الذي يرسل الرياح بشرا بين يدي رحمته حتى إذا أقلت سحابا, باللغة السواحيلية

﴿وهو الذي يرسل الرياح بشرا بين يدي رحمته حتى إذا أقلت سحابا﴾ [الأعرَاف: 57]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Ndiye Anayetuma upepo mzuri mororo wenye kubashiria mvua ambayo upepo huo unaisukuma kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na hapo viumbe vikangiwa na furaha kwa hiyo rehema ya Mwenyezi Mungu. Na pindi ifikapo wakati ambapo upepo umebeba mawingu yaliyobebeshwa mvua, Mwenyezi Mungu Huyapeleka kwa upepo huo ili kuihuisha nchi iliyopigwa na ukame ardhi yake na kukauka miti yake na mimea yake ya nafaka, Mwenyezi Mungu hapo Akaiteremsha, kwa mawingu hayo, mvua, Akaitoa kwayo nyasi, miti na mimea ya nafaka, na miti ikarudi kujaa sampuli ya matunda. Kama tunavyoihuisha ardhi hii kwa mvua, vilevile tutawatoa wafu kutoka makabarini mwao baada ya kutoweka kwao, ili muwaidhike na mchukulie dalili juu ya upweke wa Mwenyezi Mungu na uwezo Wake wa kufufua
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek