Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 56 - الأعرَاف - Page - Juz 8
﴿وَلَا تُفۡسِدُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ بَعۡدَ إِصۡلَٰحِهَا وَٱدۡعُوهُ خَوۡفٗا وَطَمَعًاۚ إِنَّ رَحۡمَتَ ٱللَّهِ قَرِيبٞ مِّنَ ٱلۡمُحۡسِنِينَ ﴾
[الأعرَاف: 56]
﴿ولا تفسدوا في الأرض بعد إصلاحها وادعوه خوفا وطمعا إن رحمة الله﴾ [الأعرَاف: 56]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Wala msilete katika ardhi aina yoyote ya uharibifu, baada ya Mwenyezi Mungu kuitengeneza kwa kutuma Mitume, amani iwashukie, na kuimarika kwa utiifu wa Mwenyezi Mungu. Na muombeni Yeye, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, mkimtakasia maombi yenu, kwa kuogopa mateso Yake na kuwa na matumaini kupata malipo Yake mazuri. Hakika rehema ya Mwenyezi Mungu iko karibu na wenye kufanya wema |