Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 73 - الأعرَاف - Page - Juz 8
﴿وَإِلَىٰ ثَمُودَ أَخَاهُمۡ صَٰلِحٗاۚ قَالَ يَٰقَوۡمِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنۡ إِلَٰهٍ غَيۡرُهُۥۖ قَدۡ جَآءَتۡكُم بَيِّنَةٞ مِّن رَّبِّكُمۡۖ هَٰذِهِۦ نَاقَةُ ٱللَّهِ لَكُمۡ ءَايَةٗۖ فَذَرُوهَا تَأۡكُلۡ فِيٓ أَرۡضِ ٱللَّهِۖ وَلَا تَمَسُّوهَا بِسُوٓءٖ فَيَأۡخُذَكُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ ﴾
[الأعرَاف: 73]
﴿وإلى ثمود أخاهم صالحا قال ياقوم اعبدوا الله ما لكم من إله﴾ [الأعرَاف: 73]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na tulimtuma, kwenda kwa watu wa kabila la Thamūd, ndugu yao Ṣāliḥ, walipoabudu masanamu badala ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka. Ṣāliḥ aliwaambia, «Enyi watu wangu, muabuduni Mwenyezi Mungu, Peke Yake, hamna mola anyestahiki kuabudiwa isipokuwa Yeye, Aliyetukuka na kuwa juu, mtakasieni ibada, nimewajia na hoja juu ya ukweli wa yale ninayowaitia kwayo. Nayo ni kuwa nilimuomba Mwenyezi Mungu mbele yenu, Akawatolea kutoka kwenye jiwe hili ngamia mkubwa kama mlivyoomba, basi muacheni ale kwenye malisho yaliyoko kwenye ardhi ya Mwenyezi Mungu, na msimfanyie lolote la kumdhuru, mkifanya hivyo, mtapatwa na adhabu iumizayo |