×

Na kwa watu wa Madyana tulimtuma ndugu yao Shua'ib. Akasema: Enyi watu 7:85 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-A‘raf ⮕ (7:85) ayat 85 in Swahili

7:85 Surah Al-A‘raf ayat 85 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-A‘raf ayat 85 - الأعرَاف - Page - Juz 8

﴿وَإِلَىٰ مَدۡيَنَ أَخَاهُمۡ شُعَيۡبٗاۚ قَالَ يَٰقَوۡمِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنۡ إِلَٰهٍ غَيۡرُهُۥۖ قَدۡ جَآءَتۡكُم بَيِّنَةٞ مِّن رَّبِّكُمۡۖ فَأَوۡفُواْ ٱلۡكَيۡلَ وَٱلۡمِيزَانَ وَلَا تَبۡخَسُواْ ٱلنَّاسَ أَشۡيَآءَهُمۡ وَلَا تُفۡسِدُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ بَعۡدَ إِصۡلَٰحِهَاۚ ذَٰلِكُمۡ خَيۡرٞ لَّكُمۡ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ ﴾
[الأعرَاف: 85]

Na kwa watu wa Madyana tulimtuma ndugu yao Shua'ib. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Hamna mungu mwengine isipo kuwa Yeye. Imekwisha kufikieni hoja wazi kutoka kwa Mola Mlezi wenu. Basi timizeni sawasawa vipimo na mizani, wala msiwapunje watu vitu vyao, wala msifanye uharibifu katika nchi, baada ya kuwa imekwisha tengenea. Hivi ndivyo bora kwenu ikiwa nyinyi ni Waumini

❮ Previous Next ❯

ترجمة: وإلى مدين أخاهم شعيبا قال ياقوم اعبدوا الله ما لكم من إله, باللغة السواحيلية

﴿وإلى مدين أخاهم شعيبا قال ياقوم اعبدوا الله ما لكم من إله﴾ [الأعرَاف: 85]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Hakika tulimtuma, kwa watu wa kabila linalokaa Madyan, ndugu yao Shu'ayb, amani imshukie, akasema kuwaambia, «Enyi wtu wangu, muabuduni Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Asiye na mshirika. Hamna mola anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Yeye, Aliyetukuka na kuwa juu. Mtakasieni ibada.Hakika imewajia nyinyi hoja, kutoka kwa Mola wenu, juu ya ukweli wa yale ninayowaitia. Watekelezeeni watu haki zao kwa kutimiza vipimo na mizani. Na msiwapunguzie haki zao mkawadhulumu. Wala msifanye uharibifu katika ardhi, kwa ukafiri na kudhulumu, baada ya kuwa imetengenezwa kwa sheria za Mitume waliopita, amani iwashukie. Hayo niliyowaitia nyinyi ni bora kwenu katika ulimwengu wenu na Akhera yenu, iwapo nyinyi ni wenye kuniamini katika yale ninayowaitia, ni wenye kuzifuata sheria za Mwenyezi Mungu kivitendo
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek