Quran with Swahili translation - Surah Al-Jinn ayat 14 - الجِن - Page - Juz 29
﴿وَأَنَّا مِنَّا ٱلۡمُسۡلِمُونَ وَمِنَّا ٱلۡقَٰسِطُونَۖ فَمَنۡ أَسۡلَمَ فَأُوْلَٰٓئِكَ تَحَرَّوۡاْ رَشَدٗا ﴾
[الجِن: 14]
﴿وأنا منا المسلمون ومنا القاسطون فمن أسلم فأولئك تحروا رشدا﴾ [الجِن: 14]
Abdullah Muhammad Abu Bakr «Na kwamba miongoni mwetu kuna wenye kumnyenyekea Mwenyezi Mungu kwa kumtii, na miongoni mwetu kuna waliopotoka walio madhalimu ambao walienda kombo na njia ya haki. Basi mwenye kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu na kumnyenyekea kwa utiifu, hao ndio walioelekea njia ya haki na usawa, wakajibidiisha kuichagua na Mwenyezi Mungu Akawaongoza kuifikia |