×

NA JUENI ya kwamba ngawira mnayo ipata, basi khums (sehemu moja katika 8:41 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Al-Anfal ⮕ (8:41) ayat 41 in Swahili

8:41 Surah Al-Anfal ayat 41 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Al-Anfal ayat 41 - الأنفَال - Page - Juz 10

﴿۞ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّمَا غَنِمۡتُم مِّن شَيۡءٖ فَأَنَّ لِلَّهِ خُمُسَهُۥ وَلِلرَّسُولِ وَلِذِي ٱلۡقُرۡبَىٰ وَٱلۡيَتَٰمَىٰ وَٱلۡمَسَٰكِينِ وَٱبۡنِ ٱلسَّبِيلِ إِن كُنتُمۡ ءَامَنتُم بِٱللَّهِ وَمَآ أَنزَلۡنَا عَلَىٰ عَبۡدِنَا يَوۡمَ ٱلۡفُرۡقَانِ يَوۡمَ ٱلۡتَقَى ٱلۡجَمۡعَانِۗ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٌ ﴾
[الأنفَال: 41]

NA JUENI ya kwamba ngawira mnayo ipata, basi khums (sehemu moja katika tano) ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na Mtume, na jamaa, na mayatima, na masikini, na wasafiri, ikiwa nyinyi mmemuamini Mwenyezi Mungu na tuliyo yateremsha kwa mja wetu siku ya kipambanuo, siku yalipo kutana majeshi mawili. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: واعلموا أنما غنمتم من شيء فأن لله خمسه وللرسول ولذي القربى واليتامى, باللغة السواحيلية

﴿واعلموا أنما غنمتم من شيء فأن لله خمسه وللرسول ولذي القربى واليتامى﴾ [الأنفَال: 41]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Na jueni, enyi Waumini, kwamba kile mlichokipata kutoka kwa adui yenu kupitia jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi mafungu manne kati ya mafungu yake matano yapewe wapiganaji ambao walishiriki vitani, na fungu moja lililosalia kati ya yale mafungu matano litagawanywa sehemu tano: ya kwanza ni ya Mwenyezi Mungu na Mtume, iwekwe kwenye manufaa ya Waislamu wote; ya pili ni ya jamaa wa karibu na Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, nao ni waliozalikana na Hashim na waliozalikana na Muttalib. Wamwekewa sehemu hiyo ya tano mahali pa sadaka, kwani sadaka si halali kwao. Ya tatu ni ya mayatima; ya nne ni ya masikini, na ya tano ni ya msafiri aliyemalizikiwa na matumizi, iwapo nyinyi mnaukubali upweke wa Mwenyezi Mungu, mnamtii Yeye, ni wenye kuyaamini yale Aliyomteremshia mja Wake Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, miongoni mwa aya, usaidizi na ushindi katika siku Aliyopambanua baina ya haki na upotofu hapo Badr, siku lilipokutana kundi la Waumini na kundi la washirikina. Na Mwenyezi Mungu juu ya kila kitu ni Mwenye uwezo, Hashindwi na chochote
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek