Quran with Swahili translation - Surah Al-Anfal ayat 43 - الأنفَال - Page - Juz 10
﴿إِذۡ يُرِيكَهُمُ ٱللَّهُ فِي مَنَامِكَ قَلِيلٗاۖ وَلَوۡ أَرَىٰكَهُمۡ كَثِيرٗا لَّفَشِلۡتُمۡ وَلَتَنَٰزَعۡتُمۡ فِي ٱلۡأَمۡرِ وَلَٰكِنَّ ٱللَّهَ سَلَّمَۚ إِنَّهُۥ عَلِيمُۢ بِذَاتِ ٱلصُّدُورِ ﴾
[الأنفَال: 43]
﴿إذ يريكهم الله في منامك قليلا ولو أراكهم كثيرا لفشلتم ولتنازعتم في﴾ [الأنفَال: 43]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na kumbuka, ewe Nabii, pindi Mwenyezi Mungu Alipokuonyesha uchache wa maadui zako ukiwa usingizini na ukawajulisha Waumini kuhusu hilo, ndipo nyoyo zao zikapata nguvu na wakawa na ujasiri wa kupigana nao. Na kama Anagalikuonyesha Mola wako wingi wa maadui zako, basi wangalisita Maswahaba wako kupambana nao, na mungalipatwa na uoga na mkatafautiana kuhusu kupigana, lakini Mwenyezi Mungu Aliepusha jambo la nyinyi kushindwa na Akaokoa na mwisho mbaya wa hilo. Hakika Yeye ni Mjuzi mno wa yaliyofichika nyoyoni na maumbile ya nafsi |