Quran with Swahili translation - Surah Al-Anfal ayat 52 - الأنفَال - Page - Juz 10
﴿كَدَأۡبِ ءَالِ فِرۡعَوۡنَ وَٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡۚ كَفَرُواْ بِـَٔايَٰتِ ٱللَّهِ فَأَخَذَهُمُ ٱللَّهُ بِذُنُوبِهِمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ قَوِيّٞ شَدِيدُ ٱلۡعِقَابِ ﴾
[الأنفَال: 52]
﴿كدأب آل فرعون والذين من قبلهم كفروا بآيات الله فأخذهم الله بذنوبهم﴾ [الأنفَال: 52]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakika yale yaliyowapata washirikina siku hiyo ndio mwendo wa Mwenyezi Mungu katika kuwatia adabu wakiukaji mipaka miongoni mwa umma waliotangulia, mfano wa Fir'awn na waliomtangulia, walipowakanusha Mitume wa Mwenyezi Mungu na wakazipinga aya Zake. Kwa hakika Mwenyezi Mungu Aliwateremshia mateso Yake kwa sababu ya madhambi yao. Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu Asiyeshindwa, ni Mkali wa mateso kwa aliyemuasi na asitubie kutokana na dhambi zake |