Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 104 - التوبَة - Page - Juz 11
﴿أَلَمۡ يَعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ هُوَ يَقۡبَلُ ٱلتَّوۡبَةَ عَنۡ عِبَادِهِۦ وَيَأۡخُذُ ٱلصَّدَقَٰتِ وَأَنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلتَّوَّابُ ٱلرَّحِيمُ ﴾
[التوبَة: 104]
﴿ألم يعلموا أن الله هو يقبل التوبة عن عباده ويأخذ الصدقات وأن﴾ [التوبَة: 104]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kwani hawajui, hawa wenye kujikalisha nyuma na kuacha kwenda kwenye jihadi na wengineo, kwamba Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Ndiye Ambaye Anakubali toba ya waja Wake, Anachukua sadaka na Anatoa malipo yake, na kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kukubali toba ya waja Wake warejeapo Kwake, ni Mwenye kuwarehemu warudipo kutaka radhi Zake |