Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 105 - التوبَة - Page - Juz 11
﴿وَقُلِ ٱعۡمَلُواْ فَسَيَرَى ٱللَّهُ عَمَلَكُمۡ وَرَسُولُهُۥ وَٱلۡمُؤۡمِنُونَۖ وَسَتُرَدُّونَ إِلَىٰ عَٰلِمِ ٱلۡغَيۡبِ وَٱلشَّهَٰدَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ ﴾
[التوبَة: 105]
﴿وقل اعملوا فسيرى الله عملكم ورسوله والمؤمنون وستردون إلى عالم الغيب والشهادة﴾ [التوبَة: 105]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na sema, ewe Nabii, kuwaambia hawa wenye kujikalisha nyuma na kuacha kwenda kwenye jihadi, «Mfanyieni Mwenyezai Mungu yale ya kumridhisha ya kumtii na kutekeleza mambo ya lazima Aliyoyaweka na kuepuka maasia. Na Mwenyezi Mungu Atayaona matendo yenu na Mtume Wake na Waumini, na yatakuwa wazi mambo yenu, na mtarejeshwa Siku ya Kiyama kwa Anayejua yaliyofichika yenu na yaliyo wazi yenu, na hapo Atawapa habari ya yale ambayo mlikuwa mkiyafanya. Katika hii kuna tishio na onyo kwa anayeendelea kwenye ubatilifu wake na ukiukaji mipaka wake |